IGP SIRRO: TUTAFUATILIA YOTE YANAYOSEMWA MITANDAONI KUHUSU REGINALD MENGI

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro amesema Jeshi lake litafuatilia kwa kina maneno yote yanayosemwa mitandaoni kuhusu Kifo cha Reginald Mengi ili kubaini kama yana ukweli wowote ili sheria ichukue mkondo wake.

IGP Siiro ametoa kauli hiyo leo baada ya kufika nyumbani kwa Dr Mengi ili kutoa Pole ya msiba.

”Mzee Mengi alikuwa mshauri mzuri sana kwenye masuala ya ulinzi na usalama pamoja na misaada midogo midogo kwa vijana wetu wanapokuwa na shida. Zaidi alikuwa ‘very humble’ mara zote alikuwa anajishusha sana.

"Yako mengi yanayoongelewa kwa sasa mitandaoni, lakini jambo la msingi tumalize kwanza msiba, hayo yanayozungumzwa mitandaoni tutafuatilia,” amesema Sirro.

==>>Msikilize hapo chini


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527