HII HAPA RATIBA YA KUPOKEA MWILI WA DR.MENGI KESHO


Ratiba ya kuupokea mwili wa Dr. Reginald Mengi, Uwanja wa Ndege wa Mwl. Julius Kambarage Nyerere imeelezwa kuwa itafanyika kesho, Jumatatu, saa 8:00 mchana.

Mwili wake utaletwa na ndege ya Shirika la Ndege la Emirates kutokea Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu (U.A.E).

Baada ya mwili kupokelewa katika Uwanja wa Ndege wa JNIA, utapitishwa maeneo ya Tazara, Buguruni, Ilala, Kigogo, Magomeni hadi Kinondoni.

Kutoka Kinondoni, mwili wake pia utapitishwa hadi katika maeneo ya Morocco, barabara ya Bagamoyo, Sayansi, Mwenge hadi katika hospitali ya Lugalo ambako mwili wa Dr. Reginald Mengi utahifadhiwa.

Ratiba hiyo itaendelea siku ya Jumanne ya Mei 7, 2019, ambapo mwili utapelekwa katika ukumbi wa Karimjee, kwaajili ya watu wote kuuaga na kisha utarejeshwa nyumbani kwake. Siku ya Jumatano mwili utasafirishwa kupelekwa Moshi Machame ambako Ibada ya mazishi itafanyika siku ya Alhamis katika kanisa la Kisereni (KKKT).

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post