ASKOFU SIMIYU AJIUA BAADA YA MKEWE KUMNYIMA CHAKULA CHA USIKU

Askofu Emmanuel Nyongesa Simiyu mwenye umri wa miaka 45 wa kanisa la Mwamba Faith by Works Ministry kutoka kijiji cha Lurambi eneo la Kiungani kaunti ya Trans Nzoia nchini Kenya ameripotiwa kujitoa uhai baada ya madai kuwa mkewe alimnyima chakula cha usiku.

Inaelezwa kuwa Askofu Nyongesa alifika nyumbani kwake Jumamosi Mei 4,2019 kutoka ziarani akihisi njaa ila mkewe hakuwa amemwandalia chakula chochote 

 Imeripotiwa kuwa Nyongesa alirejea nyumbani Jumamosi Mei 4, akihisi njaa na akiwa mchovu, alimuuliza mkewe ampatie chakula ila hakikuwepo. 

Mkewe alidai kuwa hakumuachia pesa za kununua chakula na hivyo asingeweza kumuandalia chochote.

 Akiwa mwenye hasira, Nyongesa alienda chumbani kulala bila kula chochote ila alitishia kufanya kitendo kitakachomtikisa mkewe pamoja na waumini wake.

 "Umekataa kuniandalia chakula? utajionea maajabu, nitafanya kitendo cha kusikitisha sana ambacho kitakutisa pamoja na waumini wangu," Askofu Nyongesa alisema.

Jumapili Mei 5, askofu aliripotiwa kwenda jikoni akijifanya kuwa yuwapika kiamsha kinywa na hivyo ndivyo alijiua. Mwanawe aliupata mwili wake ukining'inia kwenye paa la nyumba.
Chanzo - Tuko

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post