Makubwa Haya : MWANAMKE AJIFUNGUA SAMAKI

Wakazi wa eneo la Shariani jimbo la Kilifi wameachwa vinywa wazi  na kudai huenda ni ushirikina baada ya mmoja wao kudaiwa kujifungua 'samaki' aliyehai.


 Wakazi hao walifurika katika boma la Sarah Mbeyu Jabiri ili kujionea kioja cha kiumbe aliyetoka tumboni mwake. 

Mwanamke huyo alinza kutokwa damu kabla ya kuanza kuhisi maumivu makali ya tumboni. 

Kulingana na taarifa ya The Standard, mambo yalikuwa shwari kwa Jabiri hadi siku ya Alhamisi wakati alipoanza kutokwa na damu na kuhisi uchungu tumboni. 

"Nilianza kutokwa na damu Alhamisi na Ijumaa wiki jana. Baadaye nilianza kuhisi maumivu ya tumbo,uchungu ambao ulikuwa sawia na ule wa kujifungua. 

Uchungu huo ulipoa siku ya Jumapili ingawaje nilizidi kutoa na damu hadi Jumatano usiku wakati nilihisi uzito chini ya kitovu changu na hapo nikaanza kusukuma," Jabiri alidokeza.

 Mwanamke huyo ambaye ni mama wa watoto watano, alipigwa na butwaa baada ya kushuhudia kilichotoka katika mfuko wake wa uzazi na kwa haraka akamfahamisha mamaake ambaye anaishi katika eneo hilo. 

"Mimi sikuwa na mimba. Nilipohisi uzito huo nilikimbia kuchukua beseni ili nikitumbukize kidude hicho humo lakini kwa bahati mbaya kilinitoka na kuanguka sakafuni. Kiumbe hicho kilikuwa na macho na mkia. Nilishtuka sana kukiona," mwanamke huyo aliongeza.

 Familia hiyo inaamini kuwa Jabiri alifanyiwa uchawi. "Tulikitumbukiza kiumbe hicho katika ndoo iliyojaa maji na ghafla kikaanza kusonga ni kama kuogelea. Jambo hili sio la kawaida. Namsikitikia mwanangu," mamaake Jabiri alisema.

 Hata hivyo, afisa mkuu wa hospitali ya Kilifi Eddy Nzomo alipuuzilia mbali madai hayo na kusema kuwa mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 30 aliugua ugonjwa ulioathiri mfuko wake wa uzazi na kusababisha uvimbe maarufu kama molar pregnancy.

 Maradhi haya huwaathiri haswa wanawake walio zaidi ya umri wa miaka 35 au chini ya miaka 20.

 Aliongeza kuwa hali hiyo pia inaweza kuwaathiri wanawake waja wazito kabla ya kufikisha miezi saba. 

Kwa sasa, Jabiri amelazwa katika hospitali ya jimbo la Kilifi kwa uchunguzi zaidi wa matibabu na vile vile kuusafisha mfuko wake wa uzazi.

Via>>Tuko

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527