POLISI WAIBIWA BUNDUKI WAKIANGALIA MPIRA


Wezi wamevunja kituo cha polisi cha Kamorwon kilichopo kaunti ya Nandi nchini Kenya, na kuiba baadhi ya silaha zilikuwepo katika kituo hicho.

Taarifa kutoka Kenya ambazo zimechapishwa na jarida la Standard Digital zinasema kwamba wakati wezi hao wakifanya uhalifu kwenye kituo cha polisi, askari waliokuwepo zamu walikuwa wanaangalia mpira, sehemu ya jirani na kituo hicho., siku ya Jumanne ya April 16,2019.

Jinsi walivyogundua silaha zimeibiwa

Baada ya kurudi kituoni hapo waligundua chumba cha askari wa zamu ambacho ndicho kiliwekwa silaha kipo wazi, huku sanduku la chuma ambalo huwekwa silaha likiwa limevunjwa.

Wezi hao wameiba silaha aina ya rifle pamoja na magazine zenye uwezo wa kuweka risasi 20, na kuacha magazine 2 zenye uwezo wa kubeba risasi 17 hadi 20.

Uchunguzi juu ya tukio hilo bado unaendelea huku ikielezwa kwamba Mkuu wa Polisi eneo la Nandi, OCPD, OCS na AP Kamanda, wamefika eneo la tukio kushuhudia jinsi tukio hilo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527