TRENI YAANGUKA MOROGORO IKITOKA DAR KWENDA MWANZA


Mabehewa matano kati ya ishirini yaliyokuwa yakisafirisha shehena ya ngano kupitia reli ya kati kutoka jijini Dar-es-salaam kuelekea jijini Mwanza yakiwa yameanguka eneo la Kola Manispaa ya morogoro.
Mabehewa matano kati ya ishirini yaliyokuwa yakisafirisha shehena ya ngano kupitia reli ya kati kutoka jijini Dar-es-salaam kuelekea jijini Mwanza yakiwa yameanguka eneo la Kola manispaa ya Morogoro.
Reli ikiwa imeharibika vibaya mara baada ya mabehewa kuacha njia.
Na Hussein Stambuli, Morogoro 

Mabehewa matano kati ya ishirini yaliyokuwa yakisafirisha shehena ya ngano kupitia reli ya kati kutoka jijini Dar-es-salaam kuelekea jijini Mwanza yameanguka eneo la Kola Manispaa ya Morogoro na kusababisha uharibifu wa miundombinu ya reli eneo hilo huku baadhi ya abiria waliokuwa wakisafiri kutumia njia hiyo kukwama kwa muda. 

Akizungumzia tukio hilo Mkuu wa stesheni ya Morogoro Salvatory Kimaro amesema ajali hiyo iliyotokea majira ya saa mbili usiku na hadi sasa chanzo chake hakijafahamika na tayari wataalamu wanaendelea na kazi za kurejesha mawasiliano ya njia hiyo. 

“Taratibu nyingine ikiwemo mafundi wameshafika eneo la tukio kuweza kufanya tathmini za ujenzi na tunasafisha njia kwa kwa kutengeneza tuta ili zitakapo fika reli tuta liwe limeshaimarika na kumalizika kwa kazi hiyo kutatarajia mwenendo wa kazi za mafundi na tunatarajia kazi itafanyika haraka na kwa uhakika kupunguza usumbufu zaidi”, amesema Kimaro. 

Aidha Kimaro amefafanua kuwa kuhusu treni za abiria zilizokuwa zikitokea Dar es salaam kuelekea Kigoma, Mpanda na Mwanza zilifika mapema Morogoro jambo ambalo limesaidia kubadilishwa kwa abiria waliotoka Dar wakaingia iliyokuwa inatoka Mwanza na wale wa Mwanza wameeendelea kwenye treni iliyokuwa ikitokea Dar es salaam kuelekea Mwanza. 

wWananchi wanoishi jirani na eneo hilo wameiomba serikali kutafuta njia mbadala ya kudhibiti ajali katika eneo hilo ambalo linaonekana kuwa na kona kali na mara kwa mara limekuwa likisababisha ajali. 

“Leo hii imetokea ajali ya treni ya mizigo ni vyema eneo hili likatazamwa vyema kabla haijatokea ajali ya treni yenye watu itakuwa hatari Zaidi” amesema Jackson Isack Mwananchi .

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post