AMREF HEALTH AFRICA YATAMBULISHA MRADI WA USAFI WA MAZINGIRA MWANZA

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Shirika la Amref Health Africa- Tanzania kwa kushirikiana na Serikali mkoani Mwanza, limetambulisha mradi wa usafi wa mazingira (Pro Poor Wash Enterprise Project Mwanza), utakaotekelezwa katika kipindi cha miaka miwili katika Halmashauri za Jiji la Mwanza na Manispaa ya Ilemela.


Mradi huo unaofadhiliwa na Jiji la Madridi nchini Hispania ulitambulishwa jana ukilenga kuwafikia takribani wananchi 50,000 hususani vijana na wanawake wanaotoka katika jamii maskini kwa kuwawezesha kukua kiuchumi kupitia shughuli mbalimbali za ujasiriamali kwa kuzalisha bidhaa mbadala ikiwemo mkaa kutokana na taka ngumu na vinyesi.

Afisa Miradi ya Maji, Usafi wa Mazingira na Afya (WASH) kutoka Shirika la Amref Health Africa-Tanzania, Mhandisi James Mturi alisema mradi huo utasaidia kuondoa taka katika maeneo ya makazi ya wananchi, kuongeza kipato kwa vijana na akina mama pamoja na kupunguza milipuko ya magonjwa.

Akizugumza kwa niaba ya Katibu Tawala Mkoa Mwanza, Katibu Tawala Msaidizi Mkoa Mwanza, Mhandisi Warioba Sanya alisema mradi huo utasaidia utekelezaji wa mpango mkakati wa jiji la Mwanza wa mwaka 2004 wa kusimamia taka ngumu, kuboresha vyoo, kusimamia na kuondoa taka katika maeneo ya makazi.

Akiwasilisha mada kwa wadau waliohudhuria utambulisho wa mradi huo, Afisa Mazingira Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Fanuel Kasenene alisema Jiji hilo huzalisha zaidi ya tani 800 za taka ngumu kwa siku ambapo asilimia 74 tu ya taka hizo ndizo hukusanywa na kupelekwa dampo hivyo mradi huo utasaidia kupambana na changamoto ya uchafuzi wa mazingira.

Naye Meneja Msaidizi- Usafi wa Mazingira kutoka Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira mkoani Mwanza (MWAUWASA), Mhandisi Salim Lossindilo alisema asilimia 66 ya wakazi wa Jiji la Mwanza hawajajiunga na mfumo wa majitaka na kwamba zaidi ya asilimia 20 hawana vyoo huku zaidi ya asilimia 90 ya vyoo vikiwa nje ya mtandao wa majitaka wa MWAUWASA.


Katika kutekeleza mradi huo, elimu kuhusu masuala ya utunzaji wa mazingira itatolewa kwa wananchi hadi ngazi ya Kaya ikiwemo ujenzi wa vyoo bora, kujiunga na huduma ya majitaka (kuondoa vinyesi) pamoja na uzalishaji wa bidhaa mbalimbali za kibiashara ikiwemo gesi na mkaa kwa kutumia taka ili kuwaimarisha wananchi kiuchumi huku wakiboresha mazingira yao.
Afisa Miradi ya Maji, Usafi wa Mazingira na Afya (WASH) kutoka Shirika la Amref Health Africa-Tanzania, Mhandisi James Mturi akizungumza kwenye kikao cha utambulisho wa mradi wa Usafi wa Mazingira Jijini Mwanza.
Katibu Tawala Msaidizi Mkoa Mwanza, Mhandisi Warioba Sanya akizungumza kwenye kikao cha utambulisho wa mradi huo.
Katibu Tawala Msaidizi Mkoa Mwanza, Mhandisi Warioba Sanya akizungumza kwenye kikao hicho kilichofanyika ukumbi wa Gold Crest Hotel Jijini Mwanza.
Afisa Mazingira Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Fanuel Kasenene akiwasilisha mada kwenye kikao hicho.
Wadau waliohudhuria kikao hicho wakimsikiliza Afisa Mazingira Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Fanuel Kasenene wakati akiwasilisha mada.
Meneja Msaidizi- Usafi wa Mazingira kutoka Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira mkoani Mwanza (MWAUWASA), Mhandisi Salim Lossindilo akiwasilisha mada kwenye kikao hicho.
Mratibu wa Mradi wa Huduma Jumuishi za Kifedha Huboresha Usafi wa Mazingira na Afya (FINISH FORT), Christopher Ndangala akiongoza kikao hicho.
"Energizer time"
Wajumbe wakifurahia "Energizer Session"
Washiriki wa kikao hicho wakifuatilia mada.
Viongozi kutoka Shirika la Amref Health Africa- Tanzania wakiwa kwenye kikao hicho.
Viongozi kutoka Shirika la Amref Health Africa- Tanzania wakiwa kwenye kikao hicho.
Wadau mbalimbali kutoka taasisi za serikali na binafsi zinazohusika na masuala ya mazingira walioshiriki kikao hicho.
Tazama BMG Online TV hapa chini




Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527