SERIKALI IMEAJIRI WATUMISHI WA AFYA 52 KATIKA HOSPITALI YA RUFAA MKOA WA SINGIDA

Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.

Serikali kupitia wizara ya afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto kwa kushirikiana na ofisi ya rais menejimenti ya utumishi wa umma na utawala bora kwa mwaka wa fedha 2018/2019 imeajiri watumishi wa kada mbalimba za afya 52 katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa singida hivyo kupunguza tatizo la upungufu wa watumishi na kufikia asilimia 45.

Kauli hiyo imetolewa April 17 ,2019  bungeni jijini Dodoma na naibu wa ziri wa afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto dkt faustine ndugulile wakati akijibu swali la mbunge wa viti maalumu AishaRose ndogoli matembe lililohoji serikali inampango gani wa kuipatia hospitali ya rufaa ya mkoa wa singida watumishi wa kutosha hasa ikizingatiwa hospitali hiyo ni tegemeo la watu wengi hususani kina mama wajawazito.

Dkt ndugulile amesema kwa mwaka wa fedha 2019/2020 wizara inategemea kuomba kibali cha kuajiri watumishi 197 wa kada mbalimbali za afya kwaajili ya hospitali ya rufaa ya mkoa wa singida.

Katika swali lake la nyongeza mbunge matembe amehoji kwa kuwa hospitali ya rufaa ya mkoa wa singida inahudumia zaidi ya wagonjwa 300 kwa siku na inatoa huduma katika maeneo mawili tofauti ambayo ni hospitali ya zamani iliyopo kata ya ipembe na hospitali mpya ya rufaa iliyopo kata ya mandewa je serikali inampango gani wa kuhakikisha inapeleka fedha za kutosha ili kumaliza ujenzi katika hospitali mpya ya rufaa ya mandewa.

Akijibu maswali hayo ya nyongeza dk ndugulile amesema wao kama serikali wamezipokea hospitali hizo za rufaa za mikoa na kusudio lao ni kuhakikisha wanaziboresha ili ziweze kutoa huduma za kibingwa kama ilivyokusudiwa.

Katika hatua nyingine naibu waziri ndugulile amemuelekeza mganga mkuu wa mkoa wa geita kuhakikisha wataalamu wote wa afya waliopelekwa na serikali ambao hawapo katika kituo cha kazi ilihali wapo mjini kuhakikisha wanafika mara moja katika hospitali ya nzela wilayani geita kuanza kutoa huduma kwa wananchi


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post