MNYIKA AHOJI RIPOTI YA CAG KUTOGAWIWA KWA WABUNGE


Mbunge wa Kibamba (Chadema) John Mnyika amehoji ni kwanini Wabunge hawajagawiwa ripoti  ya uchunguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kama kanuni za Bunge zinavyosema.


 Mnyika ameyasema hayo bungeni jijini Dodoma leo Aprili 12, alipokuwa akiomba mwongozo wa Spika Utawala Bora ambapo amesema kwamba kitendo cha wabunge kutogawiwa ripoti hiyo hakiwezi kuungwa mkono na wabunge kwa kuwa kinakiuka kanuni za Bunge.

Hata hivyo, ombi hilo la Mnyika liligonga mwamba baada ya Mwenyekiti wa Bunge, Andrew Chenge kusema ripoti hizo za CAG haziwezi kugawiwa kwa wabunge kama Mnyika anavyotaka kwa kuwa kanuni haziruhusu kufanya hivyo.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527