NIGERIA WATAMBA KUITWANGA SERENGETI BOYS MCHEZO WA UFUNGUZI KESHO

Kocha Manu Garba wa timu ya Taifa Nigeria chini ya miaka 17, amesema hana presha na mchezo wao wa ufunguzi dhidi ya Tanzania.

Amesema anaifahamu Tanzania vizuri baada ya kukutana nao katika Mashindano ya Uefa Assist nchini Uturuki hivyo ana imani mchezo wao utakuwa mzuri. "Tanzania ni vijana wadogo na wanacheza mpira wa pasi nyingi, wanacheza kwa kuelewana na sio timu ya kawaida," alisema.

Ameongeza mchezo wao utakuwa mzuri kwa timu zote kuhitaji matokeo mazuri uwanjani ili kuanza vizuri Fainali hizo.

Wakati huohuo nahodha wa Nigeria, Tijani Samson amesema wamejiandaa vizuri kuweza kupata matokeo katika mchezo huo bila kuwa na wasiwasi wowote.

Na Thomas Ng'itu - Mwanaspoti

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post