MBUNGE CHADEMA AWALALAMIKIA MA RC NA WAKUU WA WILAYA WANAOWAKAMATA WANANCHI NA KUWAWEKA NDANI


Mbunge wa Rombo (CHADEMA)  Joseph Selesini   amewalalamikia baadhi ya viongozi wa Serikali wakiwamo wakuu wa mikoa na wilaya kufanya vitendo alivyoviita vya ovyo kwa wananchi.

Akiuliza swali bungeni leo, Selasini amesema anatambua juhudi mbalimbali ambazo zimekuwa zikifanywa na Serikali katika kutatua tatizo hilo.

Hata hivyo, amesema mkuu wa wilaya ya Hai amekuwa akiendelea na vitendo alivyoviita vya ovyo vya kuwakamata wawekezaji na wananchi pamoja na kushinikiza baadhi ya wanasiasa kwa kutumia askari wahame kwenye vyama vyao.

Hivyo, akahoji ni hatua gani zinachukuliwa na  Serikali kukomesha jambo hilo.

Akijibu swali hilo , Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Suleiman Jafo amesema ni kweli awali hali ilikuwa ni  mbaya kwa sababu idadi ya waliokuwa wanafanya vitendo hivyo ilikuwa ni kubwa.

“Wakuu wa mikoa, wilaya na wakurugenzi hasa wakuu wa wilaya walikuwa wakifanya mambo yasivyo lakini tunajua sisi ndani tumefanya tathimini hali imebadilika sana,” amesema.

Jafo amesema bado kuna baadhi ya kesi wanaendelea kushughulikia na hata mambo wanayozungumza (wabunge) mengine yapo katika utaratibu wa kuyashughulikia.

“Tuvute subira si kila kitu kukitangaze public  lengo letu ni utii wa sheria bila shurti kwa wananchi wote lakini kanuni na sheria kwa viongozi wote lazima zifuatwe,” amesema.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post