WATU 27 WAFARIKI DUNIA KWA KUNYWESHWA JIK NA MCHUNGAJI KANISANI



Jinsi JIK ilivyotumika

Watu takriban 27 wamefariki dunia baada ya mchungaji Rufus Phalawa kanisa la kilokole la 'AK Spiritual Christian Church' lililopo Limpopo nchini Zambia, kuwanywesha dawa ya kuondoa madoa 'jik' wakiwa kanisani.

Taarifa kutoka Zambia zilizochapishwa na jarida la Zambia Observer, zinasema kwamba mchungaji Phala aliwaambia waumini wake kuwa jik hiyo inaondoa mapepo, hivyo akaanza kuwanywesha kwa nia ya kuwaombea mapepo yao yaondoke.

Licha ya vifo hivyo, pia waumini wengine 18 hali zao si nzuri, na bado wapo hospitali wakipatiwa matibabu.

Polisi wa Limpopo wameanza uchunguzi juu ya tukio hilo, huku wakioneshwa kushangazwa kwao, ambapo miongoni mwa waliofariki, wapo wauguzi wa afya na walimu.

Source: Zambia Observer 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527