JELA MIAKA MIWILI KWA KOSA LA KUGHUSHI NA KUTUMIA VYETI BANDIA

Mahakama  ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Pwani imemuhukumu kwenda jela miaka miwili Anna Kasanda kwa kosa la kughushi na kutumia vyeti bandia.

Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Mkazi Mfawidhi wa mahakama hiyo, Rose Kangwa, alisema mahakama imeridhika na ushahidi uliotolewa na upande wa utetezi kuwa mtuhumiwa alikuwa anatumia vyeti bandia.

“Mtuhumiwa anahukumiwa kwenda jela miaka miwili kwa kosa la kwanza la kughushi leseni ya uuguzi na ukunga kinyume cha kifungu cha sheria namba 355(a) na 337 cha mwaka 2002,” alisema Rose.

Alisema kwa kosa la kujaribu kuihuisha (renew) leseni hiyo, mtuhumiwa atatumikia miaka miwili mingine. 

Rose alisema japokuwa hakuna sehemu katika ushahidi inaonesha mtuhumiwa anamiliki mashine ya kuchapa nyaraka hizo, lakini kwa mujibu wa shahidi wa pili inaonesha kuwa mtuhumiwa alitaka kuendelea kutumia vyeti hivyo.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527