MWANAFUNZI ALIYEPOTEA AKUTWA AMEZIKWA NA SARE ZA SHULE KWENYE SHAMBA LA BIBI KIZEE...WANANCHI WAUA BIBI



Tukio lisilo la kawaida limetokea Wilayani Muleba Kata ya Kishanda Mkoani Kagera ambapo mtoto mwenye miaka saba Ismail Hamisi ambaye alipotea tangu April 5,2019 akitokea shule na jana amekutwa amezikwa kwenye shamba la bibi aitwaye Coletha Francis akiwa amefukiwa kwenye shimo tayari ameshapoteza maisha.

Hali hiyo imesababisha baadhi ya wananchi wa maeneo hayo kukata migomba ya bibi huyo na kumuua kwa kumchoma moto akiwa ndani ya nyumba yake.

Kamanda wa polisi mkoani Kagera, Revocatus Malimi amesema kuwa mtoto huyo alitoweka April 5 mwaka huu alipoondoka nyumbani kwenda shule, lakini hakuonekana tena hadi mwili wake ulipogundulika umezikwa katika shamba la bibi huyo, akiwa na sare zake za shule.

Aidha Kamanda Revocatus amesema Taratibu za kiuchunguzi zaidi kuhusiana na tukio hilo zinaendelea kufanyika.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527