KAMPUNI ZILIZOINGIA MIKATABA NA MAREHEMU STEVEN KANUMBA NA MZEE MAJUTO ZAANZA KUZILIPA FAMILIA ZAO


Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe amesema Wasimamizi wa mirathi ya wasanii Steven Kanumba na King Majuto wamelipwa Tsh. Milioni 45 baada ya serikali kupitia upya mikataba yao.

Ameyasema hayo leo Bungeni akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2019/2020 ambapo ameeleza hayo ni mafanikio ya kama iliyoundwa na Serikali kufanya kazi ya kupitia upya mikataba hiyo.


Amesema kampuni ya Steps Entertainment imeshamkabidhi Mama wa  muigizaji marehemu, Steven Kanumba malipo ya ziada ya Sh milioni 15 baada ya kugundulika kuwa iliingia mkataba mbovu na msanii huyo.

Pia kampuni hiyo imeahidi kushirikiana na mama yake Marehemu Kanumba, kuandaa filamu ya maisha ya mwanawe huyo.



 Waziri Mwakyembe amesema Pamoja na malipo hayo Kampuni ya Pan African Enterprises Ltd na Ivori Iringa, zimeshaingiza kwenye akaunti maalum Sh milioni 30 kwa kazi alizotekeleza muigizaji marehemu Amri Athuman maarufu King Majuto.

Pia amesema  Kampuni ya Azam SSB imeandaa malipo ya ziada ya sh milioni 20 na Kampuni ya Tanfoam ya Arusha imeandaa Sh milioni 15 yatakayowasilishwa kwa msimamizi wa mirathi ya marehemu King Majuto


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post