Picha : MWILI WA RUGE WATUA BUKOBA...MAGARI YAMEANDIKWA PLATE NUMBER 'RIP RUGE" , "MSIBA"

TAZAMA LIVE KINACHOENDELEA BUKOBA KWENYE MSIBA WA RUGE


Mamia ya wananchi wamefurika Uwanja wa Ndege Bukoba kushiriki mapokezi ya mwili wa aliyekuwa Mkurugenzi wa vipindi na uzalishaji wa Clouds Media Group Tanzania na aliyekuwa mhamasishaji mkubwa wa vijana katika matumizi ya vipaji na fursa, Ruge Mutahaba.


Magari mawili yatakayoongoza msafara tayari yameingia ndani huku 'plate number' zikiwa na maandishi ya R.I.P Ruge.

Pia magari yatakayohusika katika msafara yamepewa namba na kuandikwa neno 'msiba,na njiani kuna vibao vinavyoelekeza eneo la msiba kwenda Kijiji cha Kiziru Wilaya ya Bukoba.

Ndege ya ATCL iliyotua uwanjani hapo na baadaye kuondoka ilikuwa na abiria ambao wengi wao hawakuondoka na badala yake kujiunga na watu waliopo kiwanjani.

Baada ya mapokezi msafara utapita mitaa mbalimbali kuelekea Kiziru ambapo ataagwa kesho Jumatatu asubuhi viwanja vya Ghmkhana na mazishi kufanyika baadaye jioni.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post