RAIS MAGUFULI AMPANGIA KITUO CHA KAZI ALIYEKUWA BOSI TAKUKURU..ATEUA MWENYEKITI WA BODI YA MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Dkt. Richard Faustine Sambaiga kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali.

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi wa Dkt. Sambaiga umeanza March 23, 2019.

Dkt. Sambaiga ni Mhadhiri Mwandamizi, Idara ya Sosholojia ya Chuo Kikuu cha DSM na anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Rukia Masasi ambaye amemaliza muda wake.

Pia Rais Magufuli kesho March 28, 2019 atamuapisha Balozi Mteule Valentino Mlowola kuwa Balozi wa Tanzania nchini Cuba.

Balozi Mteule Mlowola ataapishwa Ikulu Jijini Dar es Salaam, kuanzia saa 3:30 asubuhi.





Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527