POLISI WAZUIA MKUTANO WA ACT WAZALENDO

Jeshi la Polisi Tanzania wamezuia Mkutano wa ACT-Wazalendo kwa sababu ya kuhofia wafuasi wa CUF chini ya Profesa Lipumba kuvuruga mkutano huo. 

Mkutano huo wa ndani ulipangwa kufanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa PR Stadium uliopo karibu na Uwanja wa Taifa.

Viongozi waandamizi wa ACT Wazalendo leo Machi 27,2019 wakiongozwa na Kiongozi wa Chama Ndugu Zitto Kabwe, Maalim Seif, Naibu Kiongozi wa Chama, Duni Haji walikuwa wakitarajia kukutana na wanachama wa ACT - Wazalendo.

Viongozi wengine ambao walitarajiwa kuwa kwenye mkutano huo ni pamoja na Mwenyekiti wa chama Ndugu Yeremia Maganja, Makamo Mwenyekiti Bara Ndugu Shaaban Mambo, Katibu Mkuu, Dorothy Semu na Naibu Katibu Mkuu, Msafiri Mtemelwa pamoja na viongozi wengine wa kitaifa na wa mkoa wa Dar es salaam.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post