WALIOKUWA WAFANYAKAZI BANDARI KAVU YA AZAM ICD WATUPWA JELA

Mahakama Kuu divisheni ya Rushwa na uhujumu uchumi imewahukumu wafanyakazi wawili wa zamani wa bandari kavu ya Azam ICD kutumikia kifungo cha miaka mitatu gerezani baada ya kupatikana na hatia ya makosa ya kughushi na kuisababishia serikali hasara ya sh. Bil.12.7 na kuachiwa kwa makosa ya kutakatisha fedha na kukwepa kodi.

Pia mahakama imemuhukumu Benson Malembo mfanyakazi wa Region Cargo Service kutumikia kifungo cha miaka miwili gerezani kwa kukutwa na hatia ya kuisababishia serikali hasara ya zaidi ya sh. Bilioni 12.

Mbali na Malembo, washtakiwa waliotiwa hatiani na kusomewa Hukumu yao leo Machi 28.2019 na Jaji Winifrida. Korosso ni Raymond Adolf Louis ambaye ni Meneja wa oparesheni za usalama na Khalid Yusufu Louis.

Louis na Hassan wamehukumiwa kifungo cha miaka mitatu kila mmoja kwa kila shtaka katika mashtaka 104 ya kughushi na kifungo cha miaka miwili kila mmoja katika shtaka moja la kuisababishia Mamlaka ya Mapato (TRA) hasara ya Sh12.5 bilioni.

Akitoa adhabu hiyo, Jaji Korosso amesema adhabu zote hizo zinakwenda kwa pamoja.

Mbali na adhabu hiyo ya kifungo, pia Jaji Korosso ameamuru washtakiwa baada ya kumaliza kifungo chao kuilipa TRA fidia ya nusu ya hasara waliyoisababishia, yaani zaidi ya Sh6 bilioni wote kwa pamoja.

Malembo amehukumiwa kutumia adhabu ya miaka miwili jela baada ya kupatikana na hatia katika shtaka moja la kuisababishia TRA hasara hiyo ya Sh12.5 bilioni.

Upande wa mashtaka uliita jumla ya mashahidi 34 mahakamani hapo kutoa ushahidi wao ambapo Jaji Korosso amesema kupitia ushahidi huo, upande wa mashtaka umethibitisha kesi dhidi ya washtakiwa hao.

Hata hivyo, mahakama hiyo imewaachia huru washtakiwa waliokuwa wanakabiliwa na mashtaka hayo baada ya upande wa mashtaka kushindwa kuthibitisha mashtaka dhidi yao.

Washtakiwa walioachiwa ni, Mchambuzi Mwandamizi wa Masuala ya Biashara TRA, Hamis Omary, Haroun Mpande wa kitengo cha mawasiliano na kompyuta ICT TRA

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527