Tuesday, March 5, 2019

NYALANDU : SIKULETWA CHADEMA NA MAFURIKO...KESHO NI NZURI KULIKO JANA

  Malunde       Tuesday, March 5, 2019
Siku chache baada ya Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa kurudi CCM akitokea Chadema, Mbunge wa zamani wa Singida Kaskazini ambaye kwa sasa ni kada wa Chadema, Lazaro Nyalandu amesema hakuletwa kwenye chama hicho na mafuriko.

Lowassa aliyerejea CCM wiki iliyopita alijiunga na Chadema Julai 28, 2015 na kupitishwa kugombea urais kupitia chama hicho akiwakilisha pia vyama vya Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) akiwa na kundi kubwa la wana CCM waliohama naye wakifahamika kama mafuriko.

Hata hivyo, Nyalandu aliyejitoa CCM Oktoba 30, 2017 na baadaye kujiunga na Chadema jana alitumia akaunti yake ya Twitter kuandika ujumbe unaoelezea hatima yake ndani ya Chadema.

“Naamini katika kushiriki kuleta mabadiliko ya kweli Tanzania kupitia upinzani. Tusikate tamaa. Kesho ni nzuri kuliko jana,” alisema Nyalandu katika ujumbe huo.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post