BABA AMPA MIMBA MTOTO WAKE...HULALA KITANDA KIMOJA MKEWE NA WATOTO


Wanafunzi watatu wilayani Mkuranga mkoani Pwani ambao majina yao yamehifadhiwa wamelazimika kukatisha masom baada ya kupatiwa ujauzito huku mmoja wapo akimtaja baba yake kuhisika na ujauzito wake.

Wote ni wanafunzi wanaosoma katika shule ya msingi Kibuyuni iliyopo katika kijiji cha Mkuruwili, ambapo wawili kati yao ni wa darasa la saba na mmoja ambaye amemtaja baba yake wa kumlea kuhusika, ni mwanafunzi wa darasa la sita.

www.eatv.tv, imefika katika kijiji cha Mkuruwili na kuzungumza na wanafunzi hao ambao wanakiri kufanyiwa unyama huo huku mmoja wao akimtaja baba yake wa kufikia kuwa na tabia ya kumnyatia majira ya alfajiri pindi mama yake anapokwenda kuchota maji na kumlazimisha kushiriki tendo la ndoa huku akimtishia kumuua endapo atajaribu kumtaja.

Pia baadhi ya majirani wamesema kuwa sababu za mwanafunzi huyo wa darasa la sita kupewa ujauzito na baba yake wa kufikia ni kutokana na wazazi hao kulala kitanda kimoja na watoto wao.

Mwanafunzi mwingine amesimulia kuwa alibakwa na vijana wawili alipokuwa anakwenda shamba. Amesema walimvuta porini na kumfanyia kitendo hicho na alipopimwa shuleni na wenzake ndipo aligundulika na ujauzito.

Kwa upande wake mwalimu wa shule hiyo Bw. Warioba Joseph pamoja na Kaimu Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji wamekiri kutokea kwa tukio hilo huku wakieleza kuwa tayari hatua zimekwishaanza kuchukuliwa.
Chanzo - EATV

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post