ALAZIMISHWA KUZIKA MGOMBA WA NDIZI BADALA YA MKE WAKE


Familia moja kutoka kijiji cha Lubai kaunti ya Kakamega nchini Kenya imelazimisha mwanao wa kiume kuzika mgomba wa ndizi ili kuashiria mwili wa mke wake ambaye alitoweka miaka 13 iliyopita. 

Bernard Munase alishawishiwa na wazee wa jamii ya Waisukha kufanya sherehe za kumzika mkewe kulingana na tamaduni za jamii hiyo ili aweze kuoa mke mwingine. 

Wazee wa jamii hiyo walisema walihitajika kufanya sherehe hiyo ili kumpa fursa mwana wao kuoa mke mwingine.

Munase alisema amemtafuta mkewe kila pembe bila mafanikio na sasa hana imani tena iwapo atampata akiwa hai. 


 " Mungu alikuwa ametubariki na mtoto wa kiume kabla mke wangu kutoweka, mimi pamoja na jamaa wangu tumemtafuta kila mahali bila mafanikio," Munasea alisema. 

Baada ya sherehe hiyo, wazee hao walisema Munase sasa yuko huru kuoa mke mwingine na sasa yule mwingine wanaamini aliaga dunia.

" Sasa niko huru kujinyakulia mke mwingiine, nisingekubaliwa kuoa tena kwa sababu jamii ilidhanii mkewe wangu angejerea nyumbani siku moja, lakini baada ya sherehe hii ni wazi kuwa mkewe wangu aliaga dunia," Munase alisema. 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post