HALIMA MDEE : SIKUONA HAJA YA KUSEMA CHOCHOTE KUHUSU LOWASSA..NAJUA NAFSI YAKE INAVUJA DAMU YA USALITI

Mbunge wa Jimbo la Kawe, Halima Mdee amesema kwamba hakutoa neno lolote baada ya Lowassa kurudi kwenye Chama Cha Mapinduzi kwa kuwa anatambua changamoto anazozipitia kiongozi huyo kwa sasa.

Mdee amefunguka hayo wakati akijibu swali kuhusu maoni yake kufuatia aliyekuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA na Mgombea huyo wa Urais mwaka 2015 kwa mwamvuli wa Ukawa,kurudi CCM

"Natambua changamoto nyingi anazopitia za kifamilia na kibiashara, akalazimika kuomba po! sikuona haja ya kusema chochote nikiheshimu uamuzi wake. Najua nafsi yake inavuja damu ya usaliti kwa waliompa heshima na ‘kumrudishia uhai’" Ameandika Halima Mdee.

Edward Lowassa alirejea Chama cha Mapinduzi (CCM) Ijumaa, ya wiki iliyopita na kupokelewa na uongozi wa juu wa chama hicho akiwemo Mwenyekiti, Dk. John Pombe Magufuli.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post