Kocha mkuu wa Timu ya Taifa Tanzania ‘Taifa Stars’, Emmanuel Amunike amekitaja kikosi cha wachezaji 25 kinachojiandaa na mchezo dhidi ya Uganda. Stars inajiandaa na mchezo dhidi ya Uganda wa kufuzu mashindano ya Afrika, mchezo utakaopigwa 24 Machi katika uwanja wa Taifa.
Katika kikosi hiko Amunike amefanya mabadiliko kwa kuwatoa nyota waliokuwa katika kikosi hiko na kuingiza wengine.
Amunike amemuondoa kikosini Beno Kakolanya ambaye yupo nje ya uwanja kwa muda mrefu kutokana kuwa katika sintofahamu na klabu yake, lakini pia amemuondoa Abdi Banda, Ibrahim Ajib na Erasto Nyoni anayesumbuliwa na majeraha.
Katika nafasi hizo amewaongeza Aaron Kalambo(Tanzania Prison),Metacha Mnata (Mbao) na Suleman Salula (Malindi Fc Zanzibar). Huku katika upande wa mabeki akiwaongeza Vicent Philipo (Mbao Fc) na Kennedy Wilson (Singida Utd).