MASHABIKI WAVUNJA GETI, WAINGIA BURE UWANJA WA TAIFA


Mashabiki wamevunja geti upande uwanja wa Uhuru na NBSP kuingia kwa nguvu kwenye Uwanja wa Taifa kushuhudia mechi ya Taifa Stars na Uganda.

Nguvu ya mashabiki imewashinda polisi na walinzi wengine na kulivunja geti hilo saa 10.33 jioni hali iliyowalazimu polisi kujipanga upya kuzuia hali hilo.

Katika kipindi cha takribani dakika tano kabla ya polisi kuzuia mashabiki wengi tayari walikuwa wameingia na kwenda moja kwa moja jukwaani.

Kabla ya mashabiki hao kuvunja geti, walijazana katika Uwanja wa Uhuru katikati wakikata tiketi, lakini kutokana na wingi wao polisi wamepiga mabomu mawili ya machozi hali iliyowafanya mashabiki hao kukimbia nje.

Hali hiyo iliwafanya kujazana kando ya geti hilo na kusababisha kuwashinda nguvu huku baadhi wakikamatwa na polisi na kutupwa kwenye karandika la polisi.

Zimetumika nguvu za ziada kuwatawanya mashabiki hao wasiingie kwa polisi kukusanyana kwa wingi na kuanza kushusha vipigo ili kuzuia uingiaji wa mashabiki hao.

Mechi hiyo itakayoanza saa 12 jioni tayari robo tatu ya uwanja umekwisha kujaa.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post