Saturday, March 2, 2019

IGP SIRRO APANGUA MAKAMANDA WA POLISI...ANGALIA MAJINA YOTE HAPA

  Malunde       Saturday, March 2, 2019
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Simon Sirro amefanya mabadiliko ya kiuongozi kwa maofisa wa jeshi hilo baada ya Rais John Magufuli kufanya uteuzi wa makamishna wapya.
Akizungumza na vyombo vya habari Machi Mosi, IGP Sirro amewataja makamishna walioteuliwa na Rais Magufuli kuwa ni Charles Mkumbo ambaye anakwenda kuongoza kamisheni ya intelijensia na Liberatus Sabas ambaye anakuwa mkuu wa operesheni na mafunzo.


Wengine ni Leonard Lwabuzala ambaye ataongoza kamisheni ya fedha na logistics na Benedicto Wakulyamba ambaye anakuwa mkuu wa kamisheni ya utawala na menejimenti ya utumishi na Shaaban Mlai ambaye ataongoza kamisheni ya maabara ya uchunguzi wa kisayansi.

Mbali na makamishna hao, Sirro amefanya mabadiliko ya kiutawala kwa maofisa wa jeshi hilo; James Mushi ambaye alikuwa kamanda wa polisi mkoa wa Ruvuma anakuwa Mkuu wa Chuo cha Polisi (CCP) Moshi wakati RPC wa Njombe, Renata Mzinga akirudishwa Makao Makuu.

Sirro amewataja makamanda wapya wa mikoa kuwa ni Amon Kakwale (RPC wa Temeke), Jonathan Shana (RPC Arusha), Marwa Mahiga (RPC Ruvuma), Salum Hamduni (RPC Njombe) na Zuberi Chembela (RPC Ilala).

Viongozi wengine waliohamishwa vituo vya kazi ni Mihayo Nsekela (ofisi ya operesheni na mafunzo), Simon Haule ambaye alikuwa RPC wa Shinyanga anarudishwa Makao Makuu huku nafasi yake ikichukuliwa na ACP Richard  Abwao na Yusuph Sarungi ambaye alikuwa RPC Songwe anakuwa mkuu wa kitengo cha kushughulikia wizi wa mifugo (SPU).

Benedict Mapugila ameteuliwa kuongoza kikosi cha bandari wakati Michael Marwa anapelekwa makao makuu Zanzibar. Sirro amesema Albert Nyamhanga na Nsato Marijani wanakwenda Idara ya Wakimbizi ambayo iko chini ya Idara ya Uhamiaji.ANGALIA MAJINA YOTE HAPA CHINI

Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post