CUF YAFUNGUA KESI MAHAKAMANI DHIDI YA WALIOCHOMA MOTO BENDERA NA KUBADILISHA RANGI ZA OFISI YA CUF

Katibu mkuu wa Chama cha Wananchi CUF Khalifa Suleiman Khalifa amesema wamefungua kesi ya kiraia mahakama kuu ya Vuga visiwani Zanzibar dhidi ya wote waliofanya vitendo vya kijinai kwa kuchoma moto bendera na kubadilisha rangi za ofisi ya chama hicho.

Katibu mkuu huyo ametoa kauli hiyo jijini Dar es salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu hatua walizochukua kwa wanachama wa chama hicho waliohamia ACT Wazalendo kwa kuharibu mali za CUF ikiwemo bendera na ofisi za chama hicho.

Amesema takribani ofisi 100 za chama cha CUF zimepakwa rangi ya ACT Wazalendo hivyo hawawezi kufumbia macho hujuma hizo dhidi ya chama chao.

Katika hatua nyingine khalifa amesema wabunge wa CUF waliokuwa wanamuunga mokono maalim Seif Sharif Hamad wanatakiwa kushirikiana na chama hicho pekee na wale watakaobainika kuimarisha vyama vingine hatua za kinidhamu zitachukuliwa dhidi yao.

Kesi hiyo ya kiraia namba 19 ya mwaka 2019,imefunguliwa dhidi ya waliokuwa wanachama wa chama hicho kwa kuchoma bendera pamoja na kubadilisha rangi za ofisi za chama cha CUF visiwani Zanzibar,baada ya kuhamia chama cha ACT Wazalendo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527