MKUU WA MAJESHI AMTAKA RAIS ATANGAZE KUWA HANA UWEZO WA KUONGOZA NCHI | MALUNDE 1 BLOG

Tuesday, March 26, 2019

MKUU WA MAJESHI AMTAKA RAIS ATANGAZE KUWA HANA UWEZO WA KUONGOZA NCHI

  Malunde       Tuesday, March 26, 2019

Kiongozi wa jeshi nchini Algeria ametaka rais wa taifa hilo Abdelaziz Bouteflika kutangazwa kuwa hawezi kuongoza tena taifa hilo kutokana na sababu za kiafya.

''Ni sharti tutafute suluhu ya tatizo hili baada ya wiki ya maandamano dhidi yake. Tutafute suluhu ya tatizo hili haraka iwezekanavyo, ndani ya katiba'' , alisema Luteni jenerali Gaed Salah katika hotuba yake ya runinga.

Rais huyo tayari amekubali kwamba hatowania muhula wa tano katika uchaguzi ujao ambao umecheleweshwa.

Lakini wanaandamanaji wanamshutumu kuwa na njama ya kuongeza utawala wake wa miaka 20.

Mazungumzo yameanzishwa kujadili hatma ya siku za baadaye ya Algeria ambayo yataongozwa na mwanadiplomasia wa muda mrefu wa Umoja wa mataifa Lakhdar Brahimi.

Maandamano yalianza mwezi mmoja uliopita wakati rais huyo mwenye umri wa miaka 82 aliposema kuwa anapanga kuwania urais kwa muhula mwengine .

Lakini watu waliendelea kuandamana hata baada ya kusema kuwa hatowania tena muhula mwingine na badala yake wakataka kufanyika kwa mabadiliko ya haraka.

Luteni jenerali Gaed Salah awali alinukuliwa akisema kuwa jeshi na raia wanafikiria kuhusu hatma ya taifa hilo akitoa ishara kwamba jeshi linaunga mkono maandamano hayo.

Ni nini haswa alichosema mkuu huyo wa jeshi?

Katika hotuba yake iliopeperushwa hewani na kituo cha umma, kiongozi huyo wa jeshi na naibu wa wizara ya ulinzi alisema kuwa ''katiba ndio njia pekee ya kuleta uthabiti wa kisiasa'' .

Ametoa wito wa kutumika kwa kifungu 102 ambacho kinaliruhusu baraza la kikatiba nchini Algeria kutangaza wadhfa wa urais kuwa uko wazi iwapo kiongozi huyo hawezi kuongoza.

''Suluhu hii itavutia uungwaji mkono na lazima iungwe mkono na kila mtu'' , aliaesma Luteni jenarali Gaed Salah ambaye alipongezwa na maafisa waliokuwa wakitazama hotuba yake.

Tangazo hilo la jeshi la Algeria ni muhimu sana.
Hata hivyo, hali ya afya ya rais Bouteflika, na mgogoro wa kikatiba kuhusu utawala wake hadi uchaguzi mwengine utakapofanyika mbali na wito wa waandamanaji ambao wanasalia katika barabara za Algeria, hatua hiyo haitarajiwa kufanikiwa.

Bado kutakuwa na maswali kuhusu uamuzi huo wa mkuu wa jeshi.

Katika miaka ya hivi karibuni, ni wandani wa kisiasa na wale wa kijeshi wa rais huyo ambao wamekuwa wakizungumza kwa niaba yake huku uwepo wake ukipingua kutokana na hali yake ya kiafya.

Luteni jenerali Ahmad Gaed Salah anaonekana kuwa mtiifu sana kwa rais Bouteflika na nguzo muhimu ya utawala wa rais huyo nchini Algeria ambapo wikendi iliopita gazeti moja la kibinafsi lilitaka atimuliwe madarakani pamoja na rais huyo.

Baraza la kikatiba la taifa ilo litalazimika kuunga mkono wito wake wa hivi karibuni na baadaye itasalia kwa bunge kuamua kuhusu hatma ya rais huyo.
Chanzo - BBC
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post