CHADEMA WAFUNGUKA MAALIM SEIF KUHAMIA ACT WAZALENDO


Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, Dkt Vincent Mashinji.

Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, Dkt Vincent Mashinji amempongeza aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF kwa hatua yake ya kujiunga na Chama cha ACT- Wazalendo na kusema uamuzi wake ni sahihi.

Katibu Mkuu wa CHADEMA Vincent Mashinji 
 amesema, "nimpongeze kwa uamuzi wake wa kuendelea na shughuli za kisiasa na kupigania mabadiliko kwenye taifa letu, watu wengi walitegemea yeye kupumzika lakini amejipima na ameona anahitaji kuendelea kufanya kazi ni hatua kubwa kwetu sisi wapinzani."

Mapema leo Machi 18, 2019 Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es salaam, ilitangaza kutambua uhalali wa mwenyekiti wa chama hicho anayetambuliwa na Msajili wa Vyama vya Siasa Profesa Ibrahim Lipumba.

Kufuatia maamuzi hayo ya Mahakama majira ya saa nane leo Machi 18, 2019 alitangaza uamuzi wa kuhamia Chama Cha ACT- Wazalendo kwa kile alichokidai amesoma katiba za vyama vingine na kubaini masharti ya chama hicho ni nafuu zaidi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527