DK. BASHIRU AWATAKA CCM WASIFANYE UHUNI HUU


Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dk Bashiru Ally, amewataka wanachama wa CCM kuheshimu alama za vyama vyote vya siasa nchini kwa sababu vimesajiliwa kisheria.

Dk Bashiru amesema hayo wakati akizindua mkakati wa kukomaza demokrasia kwenye mashina ulioandaliwa na CCM mkoa wa Dodoma.

Amewataka kutochoma wala kubeza alama za vyama hivyo na kwamba huku akigusia suala la wafuasi wengine kuchoma bendera na kupaka rangi ya chama chao ofisi za chama kingine.

"CCM tusifanye mambo holela na uhuni huo katika siasa. Ni kosa kuparamia na kupaka rangi ofisi za vyama hivyo. CCM tusifanye hivyo ni kosa kisheria''. amesema.

Ameongeza, Sisi wanachama wa Chama cha Mapinduzi tunao wajibu wa kulinda uhuru wa vyama vingine vilivyosajiliwa kisheria, kama sisi tunafurahi na kuimba nyimbo zetu acheni na wao wafurahi na kuimba nyimbo zao, kama sisi tunapendeza na nguo zetu acheni na wao wapendeze na nguo zao.

Chanzo - EATV

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post