MBUNGE AZZA HILAL ACHANGIA MABATI KUSAIDIA UJENZI WA VYOO VYA SHULE ZA MSINGI "TINDE A" NA "TINDE B"


Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga,Mheshimiwa Azza Hilal Hamad (CCM) amechangia mabati 23 kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa vyoo katika shule za msingi Tinde A na Tinde B zilizopo katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga ambazo zinakabiliwa na changamoto ya uhaba wa vyoo.

Mheshimiwa Azza amekabidhi mabati hayo leo Februari 21,2019 kwa uongozi wa serikali ya kijiji cha Jomu na kamati za ujenzi za shule hiyo ikiwa ni mchango wake baada ya kuona wananchi wamejitokeza kuanzisha ujenzi wa vyoo hivyo.

Mbunge huyo alisema mabati hayo yenye geji 28,futi 10 yatatumika katika upauaji wa vyoo vya shule hizo hizo zenye jumla ya wanafunzi 2064 ambapo sasa wana matundu manne pekee ambayo nayo yamejaa.

“Mimi ni zao la Tinde, nimesomea hapa Tinde,Nimekuja kuwashika mkono kwa kuchangia mabati haya 23 ili wanafunzi wetu wasome katika mazingira bora,ni wajibu wetu sote kushirikiana ili kuboresha miundombinu ya shule”,alisema Azza.

Naye Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko aliwashukuru wananchi kujitokeza kushiriki kujenga vyoo vya shule na madarasa huku akiwakumbusha pia kujenga vyoo katika familia zao.
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga,Mheshimiwa Azza Hilal Hamad (CCM) akizungumza wakati akichangia mabati 23 kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa vyoo katika shule za msingi Tinde A na Tinde B zilizopo katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga,Mheshimiwa Azza Hilal Hamad (CCM) akiwahamasisha wakazi wa Tinde kuendelea kuchangia katika shughuli za maendeleo.
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga,Mheshimiwa Azza Hilal Hamad (CCM) akizungumza na wakazi wa Tinde.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akiwasisitiza wakazi wa Tinde kujenga vyoo kwenye shule na kwenye familia zao.
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga,Mheshimiwa Azza Hilal Hamad (CCM) akikabidhi mabati 23 kwa uongozi wa kijiji cha Jomu kwa ajili ya ujenzi wa vyoo katika shule za msingi Tinde A na B.
Zoezi la kukabidhi mabati likiendelea.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Jasinta Mboneko akiangalia vyoo vilivyochimbwa kwa nguvu ya wananchi katika shule ya Msingi Tinde A ambapo mabati yaliyotolewa na mbunge Azza Hilal yatatumika katika upauaji.
Mwenyekiti wa kijiji cha Jomu akionesha vyoo vya shule ya msingi Tinde B ambapo pia mabati yaliyotolewa na Mbunge Azza Hilal yatatumika katika upauaji.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527