RAIS MAGUFULI AMLILIA RUGE MUTAHABA....ATUMA SALAMU ZA POLE


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ametuma salamu za pole kufuatia kifo cha Mkurugenzi wa vipindi wa Clouds Media group, Ruge Mutahaba aliyefariki dunia leo wakati akiendelea na matibabu nchini Afrika Kusini akisumbuliwa na maradhi ya figo kwa miezi kadhaa.


Kupitia ukurasa wake wa Twitter ameandika ujumbe ufuatao.

"Nimepokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha kijana wangu Ruge Mutahaba. Daima nitamkumbuka kwa mchango wake mkubwa ktk tasnia ya habari, burudani, na juhudi za kujenga fikra za maendeleo kwa vijana. Poleni wanafamilia,ndugu,jamaa na marafiki. Mungu amweke mahali pema, Amina".


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post