BABU WA MIAKA 70 ASHAMBULIWA KISHA KUKATWA NYETI ZAKE NA WASIOJULIKANA

 Mzee mmoja mwenye umri wa miaka 70 aitwae  Peter Mutisya Mutongoi anaendelea kupatiwa matibabu katika hospitali ya Machakos Level Five baada ya kuvamiwa na watu wasiojulikana na kumkata sehemu zake za siri 'nyeti'.


Inaelezwa kuwa alishambuliwa akiwa katika soko la Bishop Ndingi kata ndogo ya Mwala Kaunti ya Machakos nchini Kenya mwendo wa saa tatu usiku Ijumaa, Februari 8,2019.

Afisa mkuu wa polisi eneo la Mwala Henry Kimathi alithibitisha kisa hicho na kusema mzee huyo aliokolewa na watu waliomkuta akivuja damu kwa wingi na akiwa katika hali mbaya.  

"Wafanyabiashara watatu katika soko ya bishop Ndingi walimkuta mzee huyo akivunja damu nyingi nusra ya kufa, walimchukua na kumkimbiza katika hospitali ya Machakos Level Five Hospitali," Kimathi alisema. 

 Mwanawe Mutisya alisema visa vya watu kukatwa sehemu nyeti katika kijiji hicho vimekithiri sana na wanaamini wanaofanya vitendo hivyo wanatumia sehemu hizo katika kufanya ushirikina. 

Maafisa wa polisi wameanzisha uchunguzi dhidi ya waliotekeleza unyama huo na wameahidi kuwachukulia hatua kali ya kisheria. 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post