PAPA FRANCIS AKIRI HADHARANI MAASKOFU NA MAPADRE KUWANYANYASA KINGONO WATAWA



Mtawa
Papa Francis 
Papa Francis amekiri kuwa makasisi wa kanisa katoliki wanawatumikisha kingono watawa wa kanisa hilo na kwamba tatizo hilo limekuwa likiendelea.

Papa Francis alikitaja kisa hicho wakati akilijibu swali kuhusu unyanyasaji wa kingono unaofanywa na mapadre dhidi ya watawa wakati wa kikao cha waandishi wa habari hapo jana aliporejea nyumbani kutoka Umoja wa Falme za Kiarabu. 

Ilikuwa ni mara ya kwanza ya kwa Papa Francis kukiri hadharani kuhusu tatizo la mapadre na maaskofu kuwanyanyasa kingono watawa.

 Alisisitiza kuwa kanisa katoliki limekuwa likilishughulikia saala hilo kwa muda sasa na akaapa kuchukua hatua zaidi.

Alisema kuwa mtangulizi wake Papa Benedict, alilazimika kufunga shirika la zima la watawa ambao walikuwa wakidhulumiwa kingono na makasisi.

Inaaminiwa kuwa hii ni mara ya kwanza Papa Francis amekiri hadharani kuhusu dhuluma za kingono dhidi ya watawa wa kanisa hilo kubwa zaidi duniani.

Amesema kuwa kanisa limejaribu kukabiliana na tatizo hilo na kwamba juhudi hizo bado ''zinaendelea''.

Alikiri kuwa makasisi na maaskofu wamekuwa wakiwanyanyasa watawa, na kwamba kanisa "linashughulikia suala hilo".

"Ni mpango ambao tumekuwa tukiendeleza,"alisema.

Hata hivyo Kanisa Katoliki leo limeyafafanua matamashi ya Kiongozi wa kanisa hilo Papa Francis kuhusu kisa cha kile alichokiita kuwa ni "utumwa wa ngono" katika shirika moja la watawa la kifaransa, likisema kuwa alimaanisha matumizi mabaya ya madaraka ambayo yalionekana katika matukio ya unyanyasaji wa kingono.

Mwezi Novemba mwaka jana kongamano la kimataifa la watawa wa kanisa katoliki duniani lililaani "utamaduni wa ukimya na usiri" ambao unawazuia kuzungumzia changamoto wanazopitia.

Siku chache zilizopita jarida la wanawake wa Vatican linalofahamika kama Women Church World lililaani vikali unyanyasaji huo ikiongeza kuwa katika visa vingine watawa wanalazimishwa kuavya mimba ya makasisi hao kwasababu kuwa na watoto-ni kitu kinachoenda tofauti na maadili ya ukatoliki.

Jarida hilo limesema vugu vugu la #MeToo limewasaidia wanawake wengi kujitokeza na kusimulia visa vyao.

Chanzo -DW Swahili & BBC Swahili

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527