MTOTO AUAWA KISHA KUTUPWA KWENYE DAMPO


Mtoto anayekadiriwa kuwa umri wa miezi saba amekutwa ameuawa kikatili na mwili wake kutelekezwa katika kontena la taka lililopo soko la Kihesa manispaa ya Iringa.

Akizungumza na mtandao huu Mwenyekiti wa Mtaa wa Sokoni Agustino Kimulike amesema kuwa dampo hilo linatumika na mitaa mitatu hivyo kama serikali wanaendelea kushirikiana na wananchi ili kumbaini mwanamke aliyefanya kitendo hicho.

Kwa upande wake Mtendaji wa Kata ya Kihesa, Swebe Datus amesema kuwa wananchi wanapaswa kukomesha matukio kama hayo kwani yanaleta sifa mbaya katika jamii.

Nao baadhi ya wananchi wa Mtaa huo Kata ya Kihesa wamelaani wanawake na mabinti wanaofanya vitendo hivyo kuongeza kuwa kama hawana uwezo wa kulea ni vyema wakatumia uzazi wa mpango ili kuepuka kubeba mimba zisizotarajiwa.

Mwili wa mtoto huyo umechukuliwa na jeshi la polisi kwajili ya taratibu za mazishi na kutoa wito kwa wananchi kuendelea kushirikiana na jeshi la polisi kwa lengo la kubaini mtu aliyefanya tukio hilo.


Via Nipashe

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post