Picha : NDEGE ZAGONGANA UWANJANI


Kimetokea kioja ndege   mbili  za kampuni ya Kenya Airways zilipogongana katika uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta nchini Kenya jioni ya Ijumaa, Februari 9,2019.

Imebainika kuwa ndege hizo mbili za mizigo ziligongana zilipokuwa gereji katika shughuli ya kufanyiwa ukarabati. 

Walioshuhudia kisa hicho wanadai kuwa ndege yenye usajili 5Y- KYR iliruka ikiwa ardhini, wahudumu walipokuwa wakiizuia dhidi ya kugonga ukuta, iligonga ndege nyingine yenye usajili 5Y-FFF iliyokuwa imeegeshwa.

 Hakuna aliyeriporiwa kujeruhiwa katika kisa hicho.

 Hii ndiyo mara ya kwanza ambapo kisa aina hiyo kuripotiwa kufanyika kati ya ndege za kampuni hiyo maarufu

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post