COCA- COLA YAZINDUA KAMPENI YA KUTUNZA FUKWE NA MAZINGIRA 'MCHANGA PEKEE'


Mkurugenzi Mkuu wa Cocacola, Bazil Gadzios (kulia) amesema kuwa kampeni ya hiyo ni ya pekee na tayari kampuni ya Coca-Cola Kwanza imefikia makubaliano na serikali (upande wa halmashauri) kwa kufanya usafi wa fukwe ya Coco (coco beach) kama eneo la kuanzia huku lengo ni kufikia fukwe zote zilizopo nchini Tanzania.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mheshimiwa Daniel Chongolo akiipongeza kampuni ya Coca Cola Kwanza kwa kampeni yao ya 'Mchanga Pekee'. Pia ameipongeza kampuni ya EcoAct Tanzania kwa ubunifu wa kutengeneza vibao vya alama za barabarani kutumia Plastic tofauti na chuma ambazo watu huzing'oa na kwenda kuuza vyuma chakavu.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirikisho la Viwanda Tanzania Leodegar Tenga, akitoa pongezi kwa Coca Cola Tanzania kuweza kuanzisha kampeni ya 'Mchanga Pekee' yenye lengo la kuelimisha, kufundisha na kuhimiza uhifadhi wa mazingira ya jamii zetu ikiwa imejikita katika ukusanyaji wa plastiki na usafishaji wa fukwe zetu.
Msanii na Balozi wa Coca Cola Kwanza Mrisho Mpoto (Mjomba) akitoa burudani na ujumbe kwa jamii iliyojitokeza katika zoezi la usafi.

Christian Mwijage Managing Director EcoAct Tanzania akielezea jinsi wanavyotumia Chupa za Plastic kutengenezea bidhaa mbalimbali, ikiwemo vibao vya tahadhari vya barabarani.
Mrisho Mpoto (kushoto) Basil Gadcious, Mkurugenzi mkuu wa Coca Cola Tanzania (Kati) na Tania Hamilton (Kulia) wakijadilia jambo.
Tania Hamilton, Mkurugenzi wa Taasisi ya Nipe Fagio akishiriki kusafisha fukwe ya Coco Beach jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya watu waliofika wakiendelea na usafi pembezoni mwa fukwe ya Coco Beach jijini Dar es Salaam.

Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.

Kampuni ya Coca-Cola kwanza na Kampuni Tanzu ya Coca-Cola Beverages Africa wameanzisha kampeni ya Mchanga Pekee yenye malengo na madhumuni ya kuelimisha, kufundisha na kuhimiza uhifadhi wa mazingira ya jamii zetu ikiwa imejikita katika ukusanyaji wa plastiki na usafishaji wa fukwe zetu.

Akizungumza katika uzinduzi wa kampeni ya Mchanga Pekee, Mkurugenzi Mkuu wa Cocacola, Bazil Gadzios amesema kuwa kampeni ya hiyo ni ya pekee na tayari kampuni ya Coca-ColaKwanza imefikia makubaliano na serikali (upande wa halmashauri) kwa kufanya usafi wa fukwe ya Coco (coco beach) kama eneo la kuanzia huku lengo ni kufikia fukwe zote zilizopo nchini Tanzania.

"Coca Cola Kwanza itaajiri na kuwawezesha wanawake na vijana kwa kuwapa vitendea kazi na posho ya kufanya usafishaji wa fukwe kwa kipindi chote kwa mwaka mzima kwa awamu ya kwanza ya mradi ambapo watakuwa na jukumu la msingi la kuhakikisha fukwe inakuwa katika hali ya usafi muda wote na kuhamasishautalii wa fukwe kwa kuwezesha wale wanao tembelea fukwe kufurahia mandhari ya fukwe hizo katika mazingira yalio safi na salama," amesema.

Nae Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Daniel Chongolo amesema wilaya ya Kinondoni imekuja na mpango maalum wa kuimarisha mazingira ya Bahari, tunazo na imetenga Bilioni 28 kwa ajili ya miradi miwili ya kuimarisha mazingira; zikiwemo fukwe za Osterbay zinazojumuisha eneo hili la Coco pamoja na kuimarisha mazingira ya soko la Tandale," Amesema.

Mbali na fedha hizo za miradi miwili, Serikali mwaka jana ilitoa zaidi ya shilingi Bilioni 9 kwa ajili ya ukarabati wa soko la Magomeni, Jijini Dar Es Salaam zoezi ambalo linaendeleo mpaka sasa, aidha Chongolo alitoa wito kwa jamii kuhusu kuendeleza na kuzitunza fukwe za bahari ili kutengeneza mazingira mazuri ya wananchi kupumzika pia kubarizi.

Kampeni ya Mchanga Pekee ina lengo la kutunza usafishaji wa fukwe na kuziweka katika mandhari salama,endelevu na zenya kuvutia yaani kuubakiza mchanga peke yake kwenye fukwe kwa kuondoa vitu visivyostahili kuwepo (uchafu-plastiki) na pia kampeni itajikita katika ukusanyaji wa chupa za plastiki katika mazingira yetu kuwezesha mazingira kuwa salama na yenye kuweza kuhifadhi ekolojia ya mazingira iliopo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post