MO DEWJI AWATAJA MASHABIKI WA KWELI SIMBA


Mohammed Dewji

Kuelekea mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Simba SC dhidi ya Al Ahly Jumanne ijayo, mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi Simba Mohammed Dewji, amesema mashabiki wa kweli ni wale wenye kuishangilia timu katika nyakati zote.

Ujumbe huo wa Mo Dewji anayemiliki asilimia 49 ya hisa za Simba, umekuja siku moja baada ya kuweka wazi mipango ya timu hiyo katika kuhakikisha wanafanya vizuri katika michuano hiyo.

''Nirahisi kujitokeza nakuchukua sifa iwapo Simba itashinda, lakini mashabiki wa kweli ni wale ambao wanajirudi na kushangilia Simba pindi inapopita katika kipindi kigumu. Mashabiki wa kweli wanakuwepo wakati mzuri na wakati mbaya'', ameandika Mo Dewji.

Simba ina kibarua cha kushinda mchezo huo ili iweze kufufua matumaini ya kutinga hatua ya robo fainali ya michuano hiyo, jambo ambalo Mo Dewji jana aliweka wazi kuwa linawezekana.

Mchezo huo utapigwa kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es salaam Jumanne Februari 12, 2019 kuanzia saa 10:00 jioni. Tayari viingilio vimeshatangazwa ambavyo ni 15,000, 10,000 na 2,000.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post