Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Urambo Magharibi na Waziri wa Ulinzi katika serikali ya awamu ya nne, Profesa Juma Athuman Kapuya amefunga ndoa na mpenzi wake Mwajuma Mwiniko.
Ndoa hiyo kati Prof Kapuya mwenye umri wa miaka 74 na binti huyo anayedaiwa kuwa na umri wa miaka 25 imefungwa Wilayani Urambo Mkoani Tabora siku ya jana tarehe 17 Februari, 2019