JIKO LAUA WATOTO WAWILI TARIME | MALUNDE 1 BLOG

Sunday, February 3, 2019

JIKO LAUA WATOTO WAWILI TARIME

  Malunde       Sunday, February 3, 2019
Jiko la mkaa lililokuwa ndani limesababnisha vifo vya watoto wawili baada ya kukosa hewa wakati wakiwa wamelala usiku.

Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo Jumapili Februari 3, 2019, katika mtaa wa Kebaga, wilayani Tarime mkoani Mara kwa watoto hao Witness Machugu (1) na Christina Marwa mwenye umri kati ya miaka 12-13 wakiwa wamelala chumba kilichokuwa na jiko la mkaa huku madirisha yakiwa yamefungwa.

Babu wa marehemu hao, Hobo Kihugi alisema mkwe wake aliweka jiko hilo kwenye chumba cha watoto jana usiku kwa lengo la kuandaa uji wa watoto.

Kamanda wa Polisi, Tarime-Rorya hajazungumzia tukio hili licha ya gari la polisi na askari kufika nyumbani kwa marehemu kuuchukua mwili wa Witness na kuupeleka chumba cha kuhifadhia maiti Hospitali ya Mji wa Tarime.

Mwili wa Christina ulibaki nyumbani kwa ndugu zake wakidai wanataka kuuzika kwani taratibu zote zilikuwa zimekamilika ikiwamo kuchimba kaburi. Hata hivyo, polisi wamedai haiwezekani kwani lazima uchunguzi ufanyike.

Na Waitara Meng'anyi, Mwananchi
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post