DAWASA YAJIBU KERO YA MAJI KWA WAKAZI WA MBEZI KWA MSUGULI NA VITONGOJI VYAKE


Meneja wa DAWASA- Kimara jijini Dar es Salaam Paschal Fumbuka (kulia) na Msimamizi wa Bomba kubwa la MajiSafi na MajiTaka la DAWASA Mhandishi Gibson Baragula (kushoto) wakimwonyesha mwanahabari bomba lililotobolewa ili kuweza kusambazia maji wakazi wa Mbezi kwa Msuguli jijini Dar es Salaam na vitongoji vyake. Picha zote na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.
Meneja wa DAWASA- Kimara jijini Dar es Salaam Paschal Fumbuka (kulia) wakimwonyesha mwanahabari jinsi maji yanavyotoka katika maungio ya bomba lililotobolewa ili kumaliza mgao kwa wakazi wa Mbezi wa Msuguli jijini Dar es Salaam na vitongoji vyake.

Wafanyakazi wa DAWASA wakiendelea na zoezi la uunganishaji wa mabomba.

Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.

Wakazi wa Mbezi Kwa Msuguli na vitongoji vyake jijini Dar es Salaam wanatarajia kuanza kupata maji bila ya mgao mara baada ya kukamilika uunganishwaji wa bomba jipya.

Bomba hilo jipya la Mamlaka ya MajiSafi na MajiSafi (DAWASA) litajibu kero ya mgao waliyokuwa wakipata wakazi wa Bwaloni, Msaki, Saranga, Majengo mapya mpaka Malamba Mawili, Msingwa, Kanisa la Udongo, Kisiwani na vitingoji vyake.

Akizungumza mara baada ya kumaliza zoezi la utomboaji wa Bomba, Msimamizi wa bomba kubwa la MajiSafi wa DAWASA Mhandisi Gibson Baragula amesema kwa kazi hiyo ilikuwa ni kutoa toleo la nchi 8 katika bomba kubwa la nchi 40 ambapo kazi imefanyika usiku wa kuamkia leo na zoezi hili linaenda kukamilika haraka.

"Niwaombe wakazi wa Mbezi wa Msuguli na Vitongoji vyake wavumilie tumalize ili waweze kupata ya uhakika kwa vile yatakuwa na presha ya kutosha na wataweza kupata wote kwa wakati mmoja," amesema Mhandisi Baragula.

Nae Meneja wa DAWASA- Kimara jijini Dar es Salaam Paschal Fumbuka amesema kazi kubwa imefanyika na inatarajiwa kumalizika mara baada ya masaa 48 na kuzaa matunda ili kuweza kuwapatia maji wakazi wa maeneo ya Mbezi kwa Msuguli na vitingoji vyake maji.

"Kazi kubwa ilinakaribia kukamilika na wakazi wa Mbezi kwa Msuguli wakae mkao wa kunywa maji safi na salama," amesema.

Ametoa wito kwa wakazi wote wa maeneo hayo kuendelea kuwa mabalozi wema kwa kuendelea kulipia bili zao za maji kwa wakati ili wawepe huduma bora.

"Sisi wajibu wetu tunaenda kuukamilisha hivyo basi niwaombe wale wote wanaodaiwa kulipa madeni yao na pia tutapita nyumba kwa nyumba kufanya msako wa uhakiki wa wateja, Amesema.

Maeneo ya Mbezi kwa Msuguli yamekuwa wakikosa huduma ya maji safi na salama kwa kipindi kirefu kutokana na miundombinu na jografia ya maeneo hayo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527