Picha : MBUNGE AZZA HILAL ATEKELEZA AHADI YA MCHANGO WA MABATI UJENZI WA VYOO SHULE ZA MASUNULA NA USULE


Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM),Mheshimiwa Azza Hilal Hamad ametekeleza ahadi ya kuchangia mabati 20 kwa ajili ya ujenzi wa vyoo katika shule za msingi Masunula na Usule zilizopo katika kata ya Usule halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.

Mheshimiwa Azza amekabidhi mabati hayo yenye futi 10,Februari 16,2019 kwa viongozi wa vijiji vya Masunula na Usule ikiwa ni ahadi aliyotoa Oktoba 15,2018, alipotembelea kata ya Usule na kuelezwa kuwa shule hizo zinakabiliwa na changamoto ya upungufu wa matundu ya vyoo.

Akizungumza wakati wa zoezi kukabidhi mabati lililoshuhudiwa pia na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mheshimiwa Jasinta Mboneko, Azza alisema mchango wake huo ni sehemu ya kuboresha shule ya Masunula ambayo kwa miaka mitatu mfululizo (2016,2017 na 2018) imekuwa ikiongoza kwa shule za serikali mkoa wa Shinyanga katika matokeo ya darasa la saba.

“Nilipewa malalamiko ya vyoo shule ya msingi Usule na shule ya msingi Masunula,nikaahidi kuchangia mabati 20,leo nimekuja kukamilisha ahadi yangu,hivyo nakabidhi mabati 10 yenye futi 10 kwa kila shule”,alisema.

Mheshimiwa Azza aliwataka wananchi kuacha kufanya siasa kwenye masuala ya maendeleo huku akiwahamasisha wananchi kujenga vyoo kwenye nyumba zao.

Diwani wa kata ya Usule Amina Bundala alimshukuru mbunge huyo kutekeleza ahadi yake na kuongeza kuwa tayari matundu 14 ya vyoo yamejengwa katika shule ya Masunula na sasa wanaendelea na shughuli ya kuezeka majengo ya vyoo hivyo.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Jasinta Mboneko alitumia fursa hiyo kuwahamasisha wananchi kusomesha watoto wao na kuachana na tamaa za kuwaozesha huku akiwataka kutumia fedha wanazopata kutokana na kilimo kujenga nyumba za kisasa.

 ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM),Mheshimiwa Azza Hilal Hamad akizungumza wakati wa kukabidhi mabati 20 kwa ajili ya ujenzi wa matundu ya vyoo katika shule za msingi Masunula na Usule. Kulia ni Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mhe. Jasinta Mboneko. Kushoto ni Mwenyekiti wa Kijiji cha Masunula, Kiyenze Majinge (CUF). Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM),Mheshimiwa Azza Hilal Hamad akizungumza wakati wa kukabidhi mabati 20 kwa ajili ya ujenzi wa matundu ya vyoo katika shule za msingi Masunula na Usule. 
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM),Mheshimiwa Azza Hilal Hamad akikabidhi moja kati ya mabati 20 kwa viongozi wa serikali za vijiji vya Masunula na Usule kwa ajili ya ujenzi wa matundu ya vyoo katika shule za Usule na Masunula.
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM),Mheshimiwa Azza Hilal Hamad akikabidhi moja kati ya mabati 20 kwa viongozi wa serikali za vijiji vya Masunula na Usule.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko akizungumza wakati Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM),Mheshimiwa Azza Hilal Hamad akikabidhi mabati 20 kwa ajili ya ujenzi wa matundu ya vyoo katika shule za msingi Masunula na Usule. 
Diwani wa kata ya Usule Amina Bundala akimshukuru mbunge Azza Hilal kwa kutekeleza ahadi yake ya kuwapatia mabati 20 kwa ajili ya ujenzi wa matundu ya vyoo.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko akizungumza katika eneo ambapo pamejengwa vyoo vya shule katika shule ya msingi Masunula.
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM),Mheshimiwa Azza Hilal Hamad akieleza jambo katika eneo la ujenzi wa vyoo kwenye shule ya msingi Masunula.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527