DAWA YENYE UWEZO WA KUMFANYA MTU MZEE KUWA NA AKILI ZA UJANA YAGUNDULIWA

Wataalamu wamegundua dawa yenye uwezo wa kuondoa hali ya kusahau sahau mambo inayowakumba wengi wanapoanza kuzeeka na huenda ikaingia katika maduka karibuni.

 Wakati wa 'uzeeni' – kusahau ulikoacha funguo, kusahau sura za watu na kushangaa ni kwa nini uliingia chumbani ni baadhi ya matukio ya kukera sana maishani kwa wazee wa miaka zaidi ya 50. 

Kwa kutilia maanani sehemu ya kawaida ya kuzeeka mtu, utafiti wenye matumaini makubwa umebaini kuwa, huenda karibuni kutapatikana dawa ya kurejesha seli katika hali yake ya ujanani.

Majaribio salama kwa binadamu yanatazamiwa kufanywa katika kipindi cha miaka miwili ijayo na dawa hiyo itakuwa ikimezwa mara moja kwa siku.

 Inatumainiwa kuwa, kutatolewa tembe ya kila siku baada ya utafiti huo itakayokuwa na nguvu za kufanya akili kuwa ‘changa’. Daily Mail la Alhamisi, Februari 14, liliripoti. 

Dawa hiyo iliyojaribiwa kwa kutumia panya wazee, imepatikana kuwa yenye uwezo huo na katika panya hao, tabia yao ilibadilika na kuwa kama ya panya wenye umri wa mdogo. 

Imeelezwa kuwa, wanasayansi kutoka Kituo cha Uraibu na Afya ya Akili cha Toronto, waliwasilisha utafiti wake Alhamisi, Februari 14, wakati wa Mkutano wa Kila Mwaka wa Shirikisho la Marekani la Uendelezaji wa Sayansi (AAAS) uliofanyika jijini Washington DC.
Dkt Etienne Sibille, aliyeongoza utafiti huo alisema: 'Kwa sasa hamna dawa ya kutibu dalili za kusahau zinazotokea wakati wa msongo wa mawazo, magonjwa mengine ya kiakili na uzee.' 

Dawa hiyo mpya ni aina ya ‘benzodiazepiene’ almaarufu kwa lugha ya kisayansi Valium. Lakini tofauti na Valium, yenye athari nyingi, dawa hiyo imetengenezwa kwa malengo maalum ya kuamsha seli za ubongo zilizodumaa zinazohitaji kufanya kazi ya kumbukumbu, Dkt Sibille alisema. 

 'Utafiti wetu umetambua dawa hii kuwa yenye uwezo wa kutatua hali za kawaida za uzeeni. Itajumlisha kujifunza na kumbukumbu, kupanga, kufanya uamuzi na kupanga.' alisema Dkt Sibille.

 Kulingana naye, majaribio salama kwa binadamu yatafanywa katika kipindi cha miaka miwili ijayo na dawa hiyo itakuwa ikimezwa mara moja kwa siku. 

Utafiti mwingine ni ule uliofanywa na katika utafiti huo, Daniela Kaufer wa Chuo Kikuu cha California, Berkeley ambaye aliwasilisha ripoti yake na aligundua kuwa, msongo wa mawazo huzeesha ubongo kwa kasi ya miaka 10 mbele ya umri wa kawaida.

 Mojawapo wa athari za kuzeeka kwa ubongo ni kulegea kwa vizuizi vya mishipa ya ubongo, hii ikiwa na maana kuwa, bacteria nyingi na vitu vingine vingeliweza kuchujwa huingia ndani ya ubongo.

 Uvimbe unaotokea katika ubongo huathiri mchakato wa akili, Profesa Kaufer alisema. 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527