WASHUKIWA WA SHAMBULIZI LA KIGAIDI NAIROBI WAJISALIMISHA

Watuhumiwa wa ugaidi waliokuwa wakisakwa na mamlaka Kenya wamejisalimisha.

Inaaminika kwamba walijisalimisha katika kituo kimoja cha polisi mjini Isiolo , kaskazini mwa mji mkuu wa Nairobi.

Wakati huo vikosi vya usalama nchini Kenya vinasema kuwa vimetibua shambulio katika eneo la kasakzini mashariki mwa mji wa Nairobi karibu na mpaka na Somalia.

 Mamlaka inasema kuwa wapiganaji walikuwa wamelanga kampuni mbili za ujenzi mjini Garissa.

Wanasema kuwa maafia wa jeshi wakishirikiana na wale wa polisi walijibu shambulio hilo na kuwaua takriban wapiganaji wanne.

Kenya inaendelea kukabiliana na matokeo ya shambulio katika hoteli ambapo takriban watu 21 waliuawa, kundi la alshabab kutoka Somali limekiri kutekeleza shambulio hilo.

Watu kadhaa kufikia sasa wamekamatwa kuhusiana na shambulio hilo na maafisa wa polisi wamechapisha picha za watu wengine wanane wanaosakwa.

Wakati huohuo wazazi wa watu watatu waliojisalmisha katika kituo cha polisi cha kaunti ya Isiolo wamesema kuwa wanao hawana hatia na wako hatarini.

Lakini licha ya kujisalimisha, wazazi wa washukiwa wamesema kuwa kesi zinazowakabili wanao zimekuwa zikiendelea na kwamba wamekuwa wakishirikiana na maafisa wa polisi, hivyobasi wakataka kujua ni kwa nini majina yao yalikuwa katika orodha hiyo ya magaidi wanaosakwa na serikali ya Kenya.

Chanzo:Bbc

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post