SERIKALI YAPIGA MARUFUKU WAGANGA WA MITI SHAMBA

 Serikali ya Rwanda imetangaza kupiga marufuku aina yoyote ya matangazo ya biashara ya madawa ya kijadi au asili na kuamuru vyombo vya habari vya nchi hiyo kusitisha vipindi vya waganga wa kijadi kunadi umaarufu wao.

Biashara ya madawa ya kijadi imeshamiri Rwanda na wizara ya afya inasema waganga wengi wa jadi wamekuwa wakitumia vyombo vya habari kupotosha wananchi.

Kulingana na tangazo la wizara ya afya ya Rwanda ni marufuku kutangaza biashara ya madawa kwa kutumia picha, mabango au pia kutumia vipaaza sauti barabarani kote nchini Rwanda.

Vyombo vya habari pia kama magazeti, mitandao ya kijamii , redio na televisheni vimekatazwa kupitisha vipindi na matangazo yoyote ya biashara kuhusu uganga wa kijadi.

Matangazo au vipindi kuhusu waganga na madawa ya kijadi siku hizi imekuwa biashara kubwa sana kwa karibu vituo vyote vya redio na televisheni za kibinafsi nchini Rwanda.

Baadhi wamesikitishwa na uamuzi wa wizara ya afya wa kuwakataza kutangaza biashara yao kupitia vipindi vya redio:

''Sijafurahishwa na uamuzi huu kwa sababu ingekuwa vizuri wizara ya afya kwanza ikatuuliza ukweli wa yale tunayozungumzia, halikadhalika ubora na uhalali wa madawa tunayotumia," alisema mmoja wa waganga.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527