Picha : RC SHINYANGA AZINDUA KAMPENI YA JIONGEZE TUWAVUSHE SALAMA

Mkuu wa mkoa wa Shinyanga bi Zainab Telack amezindua kampeni ya uwajibikaji katika kuzuia vifo vitokanavyo na uzazi ijulikanayo kwa jina la JIONGEZE TUWAVUSHE SALAMA.


Kampeni hiyo yenye lengo la kupunguza vifo vya kina mama wajawazito na watoto wachanga imezinduliwa leo Januari 18,2019 katika ukumbi wa mikutano uliopo katika jengo la ofisi za mkuu wa mkoa wa Shinyanga.

  katika uzinduzi huo imebainishwa kuwa   sababu za vifo hivyo  ni kutokwa kwa damu nyingi kabla,wakati na baada ya kujifungua ,kifafa cha uzazi pamoja na kupasuka kwa kizazi.

Bi Telack ametoa wito wa kuwajibika kwa wataalamu wa afya na kutoa elimu kwa jamii kuhusu utambuzi kwa kinamama wajawazito kutumia vituo vya afya licha ya changamoto ya upungufu wa vifaa tiba na dawa,jambo ambalo serikali yamkoa wa Shinyanga tayari imeendelea kutatua changamoto hiyo kwani upatikanaji wa dawa kwasasa ni asilimia 98.

“Wadau wa afya hakikisheni mnatoa elimu kwenye jamii umuhimu wa mama kujifungua kwenye vituo vya afya,hiii itasaidia kupunguza vifo vya kinamama na watoto wachanga,serikali ya awamu ya tano imejidhatiti kuwapatia huduma bora za afya kwenye jamii kwa kuboresha miundo mbinu ya huduma za afya,” alisema Telack

Mganga mkuu wa mkoa wa Shinyanga Dkt.Rashid Mfaume ametoa takwimu ya vifo vya kinamama kuanzia mwaka 2015 mpaka 2018, na kueleza idadi ya vifo vimepungua kutoka wakina mama wajawazito 60 hadi kufikia 56 mwaka 2018 huku vifo vya watoto wachanga mwaka 2015 vikiwa 1340 na kufikia 815 mwaka 2018.

“Vifo vya kinamama kwa mwaka 2015 ni 60, 2016 ni74, 2017 ni 73 na mwaka 2018 ni 56 lakini vifo vya watoto wachanga kwa mwaka 2015 ni 1340, 2016 ni 1080, 2017 ni 913 na mwaka 2018 ni 815,” alisema Mfaume.

Uzinduzi wa kampeni hiyo ya JIONGEZE TUWAVUSHE SALAMA umehudhuriwa na wadau mbalimbali wa afya wakiwemo wakuu wa wilaya,viongozi wadini,viongozi wa halmashauri zilipo mkoani hapa
Na Malaki Philipo- Malunde 1 blog
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainabu Telack akiwasisitiza wadau wa afya kushirikiana katika kuhakikisha wanatoa elimu kwa jamii juu ya afya ya uzazi na kuhakikisha akina mama wajawazito wanatumia vituo vya afya ili kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi. Picha zote na Steve Kanyefu- Malunde 1 blog

Bango lililobebeba ujumbe wa kampeni ya uwajibikaji katika kuzuia vifo vitokanavyo na uzazi mkoa wa Shinyanga.

Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Bi. Zainabu Telack (kushoto) akisoma ujumbe uliopo katika moja ya bango lililobeba ujumbe wa kampeni ya uwajibikaji katika kuzuia vifo vitokanavyo na uzazi mkoa wa Shinyanga.
Mganga mkuu wa mkoa wa Shinyanga Dkt. Rashid Mfaume akitoa takwimu za  vifo vya kinamama vitokanavyo na uzazi na   kueleza idadi ya vifo vimepungua kutoka wakina mama wajawazito 60 hadi kufikia 56 mwaka 2018 huku vifo vya watoto wachanga mwaka 2015 vikiwa 1340 na kufikia 815 mwaka 2018.
Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga Simon Haule akiwakumbusha wadau waliohudhuria katika ufunguzi wa kampeni ya  JIONGEZE TUWAVUSHE SALAMA umuhimu wa kutoa taarifa pindi wanapoona viashiria vya ndoa za utotoni zinazotajwa kuchangia vifo vitokanavyo na uzazi.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akisisitiza jambo katika ufunguzi huo. 
Mkuu wa wilaya ya Kahama Anamringi Macha akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo,ambapo alisema wadau kwa pamoja wanatakiwa  kushirikiana katika kampeni hiyo kwa kutoa elimu kwa jamii ili kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi.
Mratibu wa afya ya uzazi mkoa wa Shinyanga Joyce kondoro akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo ambapo alisema ni wajibu wa kila mwanajamii kuhakikisha mama mjamzito anafika katika kituo cha afya pindi anapobainika kuwa ni majamzito ili aweze kuchunguzwa kitaalamu ili kuhakikisha anajifungua salama.
Wadau wa afya  wakifuatilia uzinduzi wa kampeni hiyo.
Askofu wa kanisa la AIC Diosisi ya Shinyanga Zakayo Bugota akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo,ambapo amewaomba wadau kutumia vitendo zaidi kwa kuwafikia wananchi ili kuwanusuru wanawake wajawazito.
 Kikundi cha maigizo kutoka Kambarage mjini Shinyanga wakiigiza jinsi  mama mjamzito anavyopoteza maisha kutokana na kukosa huduma.
Viongozi wa dini kushoto ni Askofu wa Kanisa la KKKT Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria,Dkt. Emmanuel Joseph Makala na
kulia ni Askofu wa kanisa la AIC Diosisi ya Shinyanga Zakayo Bugota. 


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527