WATOTO 800 WAPOTEZA MAISHA,USHIRIKINA WATAJWA SHINYANGA

Mganga mkuu wa mkoa wa Shinyanga Dkt. Rashid Mfaume ameeleza Mfaume ameeleza mwenendo wa vifo vya watoto wachanga kwa miaka mitatu kuanzia mwaka 2015 mpka 2018, na kusema mwaka 2015 vifo vya watoto wachanga vilikuwa 1340 na mwaka 2018 kushuka hadi 815 .


Amesema vifo hivyo vinasababishwa na mzazi kutokwa na damu nyingi wakati wa kujifungua,kifafa cha uzazi na kupasuka kwa kizazi jambo ambalo baadhi ya wanajamii wamekuwa wakidhani kurogwa na kuamua kutafuta matibabu kwa waganga wa jadi badala ya kwenda kwenye vituo vya afya kupata matibabu ama ushauri kutoka kwa wataalamu wa afya.

Amesema serikali imekuwa na juhudi za kuzuia vifo vinavyosababishwa na uzazi kwa uboreshaji wa miundombinu katika sekta ya afya kutokana na juhudi za uboreshaji wa miundombinu katika sekta ya afya licha ya changamoto  zinazojitokeza ikiwemo ukosefu wa elimu kuhusu afya ya mama na mtoto.

 “Kuna vifo vingi vinavyosababishwa na uzazi vinatokana na baadhi ya vituo vya afya kukosa vitendea kazi , na wengine kuwa na tatizo la upungufu wa damu,hivyo wadau wa afya tukishirikiana kwa pamoja kuhamasisha jamii kujua umuhimu wa mama mjamzito kujifungua katika vituo vya afya itasaidia kupunguza vifo hivyo,” alisema Dkt. Mfaume

Na Malaki Philipo - Malunde1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527