TETESI ZA SOKA ULAYA ALHAMISI JAN,3 2019, OZIL KUBAKI ARSENAL


Christian Eriksen anagoma kutia saini mkataba mpya Tottenham, huku mkataba wa sasa wa kiungo huyo wa kati wa Denmark mwenye miaka 26 ukitarajiwa kufikia kikomo baada ya miezi 18. (Evening Standard)

Juventus wamethibitisha kwamba wameonyesha nia ya kumtaka kiungo wa kati wa Arsenal Aaron Ramsey, 28, bila kulipa ada yoyote baada ya mkataba wake kumalizika mwisho wa msimu. (Sky Sports) 

Wolves wamewasilisha ofa ya £18m kumtaka mshambuliaji wa Chelsea Tammy Abraham, 21, ambaye kwa sasa yupo kwa mkopo katika klabu ya Aston Villa inayocheza ligi ya Championship. (Sun)

Tammy Abraham
Mesut Ozil, 30, amesisitiza kwamba mustakabali wake bado upo Arsenal licha ya kutafutwa na Real Madrid na Inter Milan. (Goal) 

Watford hawataki kumuuzaAbdoulaye Doucoure, 26, ambaye thamani yake inakadiriwa kuwa £50m kwa Paris St-Germain wakati wa dirisha la uhamisho wa wachezaji la Januari. (Evening Standard)

Bayern Munich wameimarisha ofa yao hadi £30m wakitaka kumnunua winga wa Chelsea Callum Hudson-Odoi, 18, baada ya ofa yao ya awali ya £20m kukataliwa. (Sun)

Callum Hudson-Odoi alijiunga na Chelsea mwaka 2007

Everton wanamtaka winga wa Barcelona Malcom, ambaye amekuwa hachezeshwi sana kikosi cha kwanza tangu ajiunge na Barca kutoka Bordeaux mwanzoni mwa msimu. (Marca)

Lakini Toffees wanakabiliwa na ushindani kutoka kwa klabu ya Guangzhou Evergrande inayocheza Ligi Kuu ya Uchina, ambao wametoa ofay a euro 50m (£45m) kumtaka Mbrazil huyo. (Goal) 

Bournemouth watamruhusu mshambuliaji wa England Jermain Defoe kuondoka klabu hiyo Januari. Mchezaji huyo wa miaka 36 amechezeshwa mara nne pekee kama nguvu mpya ligini msimu huu. (Sky Sports)

Chelsea wanapanga kuendelea kuimarisha kikosi chao mwezi huu hata baada ya kumnunua Christian Pulisic. The Blues bado wanamtaka mshambuliaji wa Bournemouth Callum Wilson, 26, na pia wanamtafuta beki mpya. (Mirror)

Liverpool wanapanga kumpa mshambuliaji wa wao Daniel Sturridge, 29, mkataba mpya. (Mail)

Arsenal wamewasilisha ofay a euro 16m (£14m) kumtaka kipa wa Real Madrid kutoka Costa Rica Keylor Navas, 32. (Sport)

Kipa wa Costa Rica Keylor Navas

Newcastle wanatarajiwa kuwasilisha ofa kumtaka beki wa AC Milan kutoka Uruguay Diego Laxalt, 25, ambaye hucheza kama beki wa kushoto mwezi huu. (Calciomercato)


Manchester City hawatatafuta mchezaji wa kujaza pengo lililoachwa na kiungo wao wa kati mkabaji Fernandinho, 33, wakati wa dirisha la kuhama wachezaji Januari. (ESPN) 

Burnley na Cardiff wanang'ang'ania kupata saini ya kiungo wa kati wa Scotland Matt Phillips, 27, kutoka klabu ya West Brom inayocheza ligi ya Championship. (Mirror)

Meneja wa Monaco Thierry Henry anamtaka beki wa kati anayechezea Crystal Palace Mamadou Sakho, 28, pamoja na kiungo wa kati wa Chelsea Cesc Fabregas, 31, mwezi huu. (Independent)

Cesc Fabregas

Kiungo wa kati wa Leicester City Vicente Iborra, 30, anasema huenda akaihama klabu hiyo na kujiunga na Villarreal mwezi Januari. (RNE, via Leicester Mercury)

Mshambuliaji wa Italia Manolo Gabbiadini, 27, anataka kuihama Southampton mwezi huu, na tayari AC Milan wanamtaka. (Calciomercato)

Meneja wa Newcastle Rafael Benitez hataki kumwacha winga Jacob Murphy, 23, aondoke kwa mkopo hadi klabu hiyo itakapokuwa imepiga hatua katika kuwanunua wachezaji wengine Januari. (Chronicle)


Liverpool waliamua hawamtaki tena Christian Pulisic aliyenunuliwa na Chelsea kutoka Borussia Dortmund baada yao kumnunua Xherdan Shaqiri, 27, kutoka Stoke mwanzoni mwa msimu. (Liverpool Echo) 

Diego Godin na Atletico Madrid wanazozana kuhusu mkataba mpya na raia huyo wa Uruguay mwenye miaka 32 ambaye ni mkabaji wa kati huenda akaihama klabu hiyo mkataba wake wa sasa utakapomalizika mwisho wa msimu. (Marca)

Diego Godin

Real Madrid wanamtaka kiungo mshambuliaji wa Sevilla Pablo Sarabia, 26, ambaye amesalia na miezi 18 pekee katika mkataba wake wa sasa. (AS)

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post