MAAFANDE WA JKT TANZANIA WAPIGISHWA KWATA NA WAPIGA DEBE WA STAND SHINYANGA

Wapiga Debe wa Stand,timu ya Stand United al Maarufu kwa jina la Chama la Wana imemaliza mzunguko wa kwanza wa ligi kuu soka tanzania bara msimu wa 2018/19 kwa kuwapigisha kwata maafande wa JKT Tanzania kwa kuwachapa bao 1-0. 


Mchezo huo wa ligi kuu soka Tanzania bara umepigwa leo Januari 2  2019 katika uwanja wa CCM Kambarage mjini Shinyanga mchezo ambao haukuwa na kasi wala mvuto wowote kwa watazamaji katika kipindi cha kwanza kutokana na wachezaji kukosa utulivu uwanjani (butua butua) kwa wachezaji kushindwa kumiliki mpira hata kuchungulia nyavu zao. 

Lakini kipindi cha pili baada ya mabadiliko ya baadhi ya wachezaji kutoka timu zote mchezo ulishika kasi na wapiga debe wakafanikiwa kuwapigisha kwata maafande wa JKT Tanzania kupitia mchezaji wake Moris Mahela mnamo dakika ya 77 bao ambalo limedumu na kuwaibua vifua mbele wapiga debe haona kufikisha jumla ya alama 22. 

Kocha wa JKT Tanzania,Bakari Shime amesema makosa yaliyojitokeza katika nafasi ya ushambuliaji ndio yamesababisha kukosa alama tatu na kwamba watajipanga katika mzunguko wa lala salama. 

"Kimsingi wachezaji wameshindwa kutumia nafasi tulizopata,ambapo wenzetu wamepata nafasi moja na kuitumia kupata alama tatu,sisi tunaendelea kujipanga na michezo mingine ili kupata matokeo mazuri uwanjani", amesema Shime.

Upande wapili kwa wapiga debe huku ni hoya hoya kwani chama la wana limekuwa likisuasua kupata matokeo mazuri katika dimba la kambarage kocha Athuman Bilal amesema kazi imeanza na timu ipo tayari kuleta ushindani katika mzunguko wa pili. 

Na Malaki Philipo, Malunde 1 blog.
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post