CHELSEA YAMSAJILI MSHAMBULIAJI KINDA WA DORTMUND


Klabu ya Chelsea imemsaini mshambuliaji wa Borussia Dortmund Christian Pulisic kwa dau la Yuro 64m lakini itamtoa kwa mkopo kwa klabu hiyo ya Ujerumani hadi mwisho wa msimu.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20 raia wa Marekani , ambaye alikuwa amehusishwa na vilabu vya Liverpool na Arsenal , alijiunga na Dortumund akiwa mchezaji mchanga 2015.

Pulisic amefunga magoli tisa katika mechi 23 akiichezea Marekani.

''Ilikuwa ndoto ya Christian kujiunga na ligi ya Uingereza'' , alisema mkurugenzi wa klabu ya Dortmund Michaek Zorc.

Hiyo ni kutokana na mizizi yake ya Marekani na kutokana na hilo tulishindwa kuongeza mkataba wake.

''Kutokana na hali hiyo tumekubali ombi zuri la Chelsea''.

Kandarasi ya Pulisic katika klabu ya Dortmund ilitarajiwa kukamilika kufikia 2020.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post